Mgombea wa Ubunge tiketi ya CCM alichokisema kuhusu Wana Jija

Maswa Magharibi Mkoani Simiyu. Mgombea ubunge leo Tarehe 5/10/2020 saa 10 akiwa katika mkutano wa hadhara wa kumuombea kura mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Kushukuru kwa Diwani wa Kata ya Jija kupita bila kupigwa na kusubiri kuapishwa na kuanza kazi ya kuwatumikia wana Jija.

Amesema kuwa hapa Jija kulikuwa na Zahanati ila ilikuwa haina wodi ya Wamama lakini sasa imekamilika. Pia Kule Igunya mlitaka kuwepo na wodi yakina Mama lakini kwa kuwa serikali ya CCM ni sikivu imetekelezwa na kumalizika.
 
Mradi wa Maji ndani ya kata ya Jija ambao ulikuwa kero kwa wana Jija na hapo nyuma haukuweza kukamilika kwa Miaka minane iliyopita ila baada ya kunipa kazi nimeifanya kikamilifu na mradi umekamilika Ilobi na Jija Sekondari wana kunywa maji. sasa tumebakiza kusambaza maeneo mbalimbali ya kata hii ya Jija.
 
Katika mkutano huo uliofanyika kata ya Jija Mgombea Ubunge Ndugu Mashimba Ndaki amewaomba wananchi wa jimbo hilo kuendelea kuichagua CCM kwani ndicho chama kinachowajali watanzania bila ya ubaguzi wa aina yoyote na kipo tayari kuwatumikia na kuzilinda rasilimali za nchi kwa faida ya wote.









Comments