Ziara ya kumnadi mgombea Ubunge jimbo la Maswa Magharibi na Komredi Kheri James Mwenyekiti UVCCM Taifa hii leo

 Maswa Magharibi Mkoani Simiyu. Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi Taifa na Mlezi wa mkoa wa simiyu Komredi Kheri James leo saa 3 Asubuhi amehutubia mkutano wa hadhara wa kumuombea kura mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli pamoja na mgombea Ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Ndugu Mashimba Ndaki

Katika mkutano huo uliofanyika kata ya Masela, Komred Kheri amewaomba wananchi wa jimbo hilo kuendelea kuichagua CCM kwani ndicho chama kinachowajali watanzania bila ya ubaguzi wa aina yoyote na kipo tayari kuwatumikia na kuzilinda rasilimali za nchikwa faida ya wote.

Amesema CCM kwa miaka yote ya uongozi wake tangu Tanzania ipate uhuru, imeendelea kutatua kero  na changamoto mbalimbali za watanzania kwa kujali umoja na mshikamano bila kuwa na matabaka ya aina yeyote.







Comments