Maswa, Mkoa wa Simiyu
Mgombea Ubunge Jimbo la Maswa Magharibi Ndugu Mashimba Ndaki leo Tarehe 7/10/2020, Saa 8 mchana amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Kadogo kijiji cha Malekano, katika hadhara hiyo.
Amewaahidi wananchi wa kata ya Kadoto kijiji cha Malekano kuwa kama watamchagua na kumchagua Rais John Magufuli kuwa Rais wao. Atahakikisha anatatua kero ya maji na kuwaondolea hadha kwa kufuata maji mbali kwa kuwa kisima kilichopo kina maji yakutosha hivyo akipata ridhaa atahakikisha kuanza na kufunga pump na kujenga kisima kikubwa ili kuwezesha maji kusukumwa na kuweza kuwafikia wananchi wote wa vitongoji vya kijiji cha Malekano.

Comments
Post a Comment