Ufunguzi wa kampeni jimbo la Maswa Magharibi na Mbunge Mashimba Ndaki amewaomba wananchi kura za kutosha za Rais,Mbunge na Madiwani
Katika Ufunguzi wa kampeni jimbo la Maswa Magharibi katika kata ya Malampaka mgombea ubunge Mashimba Ndaki, alieleza kutekeleza Ilani ya CCM jimboni kwa upande wa sekta ya afya, lengo kuu lilikuwa kuboresha huduma za afya jimboni kwa wananchi wote hususani wanawake na watoto.
Uboreshaji wa kituo cha afya Malampaka umekamilika. Serikali ilitoa milioni 500 ili kukiboresha kituo hiki na kazi zifuatazo zimekamilika: Jengo la upasuaji limekamilika. Jengo la wodi ya kawaida limekamilika. Chumba cha maabara kimekamilika.
Jengo la nyumba ya mtumishi limekamilika. Jengo la kuhifadhia maiti nalo limekamilika. Kukamilika kwa uboreshaji wa kituo hiki utapunguza kwa kiasi kikubwa vifo vinavyotokana na uzazi kwa wanawake lakini pia kupata huduma za upasuaji karibu badala ya kusafiri umbali mrefu. na shughuli zote hizi zimefanyika ndani ya miaka mitano tu. Hivyo wananchi tarehe 28/10/2020 Chagua Magufuli, Chagua Mashimba na Diwani wa kata hii Mama ya Malampaka.
Pichani upande wa kulia ni Mgombea Udiwani Mashara wa kata ya Malampaka na Mgombea Ubunge akimnadi ili wananchi wachague chama cha mapinduzi ili kazi iendelee na changamoto zilizo baki kumalizwa katika awamu ijayo.

Comments
Post a Comment