Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), akizungumzia
matarajio ya wabunge katika utekelezaji wa miradi ya ubia kati ya Sekta
ya Umma na Binafsi katika kuchochea maendeleo, wakati wa semina kwa
wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na kamati ya
Uwekezaji Mitaji ya Umma, iliyofanyika Jijini Dodoma.
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
WAJUMBE wa Kamati
za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji na
Mitaji, wameishauri Serikali kutekeleza kwa vitendo miradi mikubwa na
yenye tija kwa Umma kwa kutumia njia ya Ubia kati ya Umma na Sekta
binafsi ili kuchochea haraka maendeleo ya nchi.
Inaendelea ....... . ..
Inaendelea ....... . ..
Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki amesema
kuwa wabunge wameridhishwa na na hatua zinazochukuliwa na Serikali
katika kuhakikisha kuwa mpango wa ubia kati ya Serikali na sekta binafsi
unafanikiwa na unachochea maendeleo ya wananchi.
“Kama wabunge tungependa
kuona mpango unaingizwa katika mipango ya Serikali ili kuharakisha
miradi ya maendeleo na pia tunapongeza hatua zilizochukuliwa na Serikali
ikiwemo kumteua Kamishna anayeshughulikia miradi ya ubia kati ya sekta
binafsi na ile ya umma, “ Alisisitiza Mboya
Alibainisha kuwa jukumu
la Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji
wote watakaojitokeza kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi
ya maendeleo hapa nchini.
Mwenyekiti wa Bunge
ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mhe. Endrew Chenge amesema kuwa nchi
nyingi Duniani zimefanikiwa kuwaletea wananchi wake maendeleo kupitia
utaratibu huo ambapo jambo la muhimu ni kufanywa kwa maandalizi ya kina
na kuwepo kwa utashi kutasaidia kufanikiwa kwa miradi husika .
Aliongeza kuwa mwaka huu
Serikali imeleta Bungeni Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya PPP
utakaojadiliwa na wabunge katika Bunge linaloanza Septemba 4 mwaka huu,
pamoja na mambno mengine Muswada huo unapendekeza kuanzishwa kwa Kituo
cha PPP chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, ambacho kitakuwa na jukumu
la kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayo husu miradi mbalimbali
itakayowasilishwa kwa mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi
Akizungumza katika Semina
hiyo, Kamishna wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara
ya Fedha na Mipango, Dkt. John Mboya amesema kuwa Dhamira ya Serikali ni
kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi katika kutekeleza miradi ya
ubia na Sekta binafsi ili kuleta mageuzi katika maisha ya wananchi.
“Lengo la kuwa na miradi
ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi ni kutekelezaIilani ya Chama
cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza mpango wa maendeleo na hatimaye kutoa
huduma bora kwa wananchi,” Alisisitiza Mboya
Akifafanua Mboya amesema
kuwa moja ya hatua za maboresho zilizochukuliwa na Serikali ni kuhamisha
Kituo cha kusimamia miradi ya ubia katika ya Umma na Sekta binafsi
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuja Wizara ya Fedha.
Akizungumzia majukumu ya
chombo cha kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo Dkt. Mboya amesema kuwa
chombo hicho kimepewa jukumu la kufanya uchambuzi wa kina kuhusu miradi
yenye sifa na kusimamia mchakato wa uteklezaji wa mpango huo kwa
kufuata ngazi zote zilizopo hadi utekelezaji wa mradi husika.
Aliongeza kuwa ili
kufanikisha mpango huo Serikali inasisistiza uwazi, uwajibikaji na
utayari hali itakayo sababisha kufikiwa kwa malengo ya miradi ya ubia
kati ya sekta hizo mbili ambapo alitaja baadhi ya miradi
itakayotekelezwa ambayo upembuzi yakinifu umekamilika kuwa ni ile ya
ujenzi wa Viwanda vya dawa, usambazaji wa gesi majumbani katika Jiji la
Dar es Salaam, Mtwara , Lindi na ule wa uendeshaji wa mabasi ya mwendo
kasi Jijini Dar es Salaam ambao umeanza na uko katika hatua mbalimbali
za uendelezwaji.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu
amesema kuwa tayari Bohari hiyo imekamilisha upembuzi yakinifu wa mradi
wa ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba vinavyotokana na malighafi
zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo pamba na kufikia machi mwakani zabuni
ya mradi huo itatangazwa ili kuwapata wabia.
Katika kutekeleza mradi
huo kiwanda cha kuzalisha maji ya dripu yanayotumika kwa wagonjwa
mahosipitalini pia kitajengwa ambapo kwa sasa maji hayo yanaagizwa
kutoka nchini Uganda na kwamba hatua hiyo itapunguza gharama za Serikali
za kuagiza dawa na vifaa hivyo kutoka nje ya nchi ambapo zaidi ya
shilingi trilioni 1.8 hutumika kuagiza bidhaa hizo kila mwaka.
Kwa upande wake.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC)
Mhandisi Kapuulya Musomba amesema kuwa mradi wa kusambaza gesi
majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara na Lindi unaotarajiwa
kuhgaribu zaidi ya shilingi bilioni 300, utaleta mageuzi kwa wananchi wa
mikoa hiyo ambapo wananchi zaidi ya 120,000 katika Jiji la Dar es
Salaam watafikiwa.
Aliongeza kuwa
katika mikoa ya Lindi na Mtwara wananchi zaidi ya 5,000 wataunganishiwa
gesi majumbani mwao huku viwanda zaidi 30 katika maeneo ya mradi
vitaunganishiwa huduma hiyo pamoja na vituo vya kujaza gesi kwenye
magari yanayotumia nishati hiyo.
Semina kwa wabunge wa
Kamati za Bajeti, Miundombinu na ile ya Uwekezaji Mitaji imefanyika
Jijini Dodoma ikiwashirikisha wajumbe wa Kamati hizo ili kuwajengea
uwezo wa namna dhana hiyo inavyoweza kuleta maendeleo hapa nchini.
Comments
Post a Comment