Mbunge akiwa katika vijiji vya Ngazu,Ilamata na Mwabujiku katika kuleta maendeleo Jimboni.

Mhe: Mashimba Ndaki akiwa na wananchi wa kijiji cha Ngazu alipokwenda kufanya mkutano nao ili kuanzisha shule ya msingi. Katika Kijiji hiki hakina shule kabisa watoto wanatembea kilomita 12 kwenda na kurudi shuleni,Mhe: Mbunge Ndaki aliguswa na kutoa mifuko 50 ya simenti ili kuunga mkono jitihada za wananchi.

Huduma ya maji kijiji cha Ilamata imesogezwa karibu kwa juhudi za mbunge Mashimba Ndaki katika kutimiza ahadi alizozi ahidi.
Kijiji cha Mwabujiku kina shule ya msingi iliyokuwa na vyumba vya madarasa vinne tu darasa la kwanza mpaka la saba. Tumetembelea hapo kuona jinsi walivyoongeza vyumba vingine viwili vya madarasa kwa msaada wa mbunge baada ya kuwapa mifuko 50 ya simenti na kutoa shilingi milioni sita kutoka mfuko wa jimbo la Maswa Magharibi.

Comments