MBUNGE Mashimba Ndaki (CCM), ameeleza kipaumbele chake kwa sasa katika jimbo lake kuwa ni elimu kwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo wa yote.
Alikuwa akizungumza juzi Maswa Magharibi wakati wa ziara yake jimboni kufuatilia na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Mashimba Ndaki alisema elimu ni muhimu katika kusukuma maendeleo na kwa sasa nguvu yote ni wanafunzi kusoma.
Alisema kusomesha vijana ni uwekezaji mzuri kwa vile baadaye watakuja kusaidia masuala ya maendeleo jimboni na Tanzania kwa ujumla.
Mbunge huyo alisema kwa sasa kasi kubwa ni kuhakikisha elimu inasimama kwa kuwa shule nyingi zimekuwa zikifanya vibaya.
"Kwa sasa mimi kipaumbele changu ninachokwenda nacho ni elimu … kuna watu wanakuja na maombi mengine lakini mimi naona twende kwanza na elimu na hayo mengine tutakuja kuyafanya baadaye,"
Pia Alitoa mchango wakufanikisha ujenzi wa shule na kutoa motisha kwa Waalimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao
Picha na matukio

















Comments
Post a Comment