Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF na kuvunja Bodi yote

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 21 Septemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Prof. Hasa Mlawa kuanzia leo.


Pamoja na kutengua uteuzi wa Prof. Hasa Mlawa, Rais Magufuli amevunja Bodi ya Udhamini ya Mfuko huo.


Uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Udhamini ya LAPF utafanywa baadaye.



Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam



21 Septemba, 2016

Comments