Skip to main content
Dr John Pombe Magufuli Ametaganzwa kuwa Ndie Mshindi Kwa Kiti Cha Urais Tanzania
Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara (NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji
Damian Lubuva imemtangaza Rasmi mgombea Urais wa CCM, Dr John
Pombe Magufuli kuwa mshindi halali wa kiti cha Urais katika
uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumapili wiki iliyopita.
Kwa Mujibu wa jaji Lubuva, Dr magufuli amepata ushindi wa kura
Milioni 8 ( 8,882,935 ) sawa na asilimia 58.45% huku akimwacha
kwa mbali mpinzani wake wa karibu, Edward Lowassa (Chadema)
ambaye amepata jumla ya kura Milioni 6 ( 6,077,848 ) sawa na
asilimia 39.97%
Comments
Post a Comment