HATIMAYE NAPE ALIWEKA HADHARANI ORODHA YA MAJINA YA AMBAO KUPITIA VIKAO HIVYO CCM IMEWATEUA KUGOMBEA UBUNGE NA UWAKILISHI WA MAJIMBO NA VITI MAALUM KATIKA UCHAGUZI WA OKTOBA, MWAKA 2015
CHAMA
Cha Mapinduzi leo kimemaliza Kikao chake cha Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC), kilichoanza jana, kufanya kazi ya kuteua wagombea ubunge na
uwakilishi katika majimbo yote nchini.
NEC imefanya uteuzi huo, huku majimbo 11 kati ya 240 yaliyopo nchini ikiwa imeyaweka kiporo cha kusubiri maamuzi yake kutolewa Agosti 17, mwaka huu katika kikao kingine kitakachofanywa na Kamati Kuu Maalum ya CCM.
Kuwekwa kiporo kwa majimbo hayo 11, kumetokana na sababu mbalimbali ikiwemo yaliyolazimika kurudia kura za maoni kutokana na kutokeza kasoro tofauti tofauti.


Comments
Post a Comment